• Jumatatu – Ijumaa Saa 1:30Asb – 9:30Alasiri

  • WALIOTEMBELEA

  • Ukaguzi wa Ndani

    KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI

    MAJUKUMU NA UTENDAJI WA KITENGO 

    Kipengele Na. 28 cha Kanuni za Fedha za Umma (2004) na Mwongozo wa Ukaguzi wa Ndani kipengele cha 2.3 wa Mwaka 2013 inamtaka Afisa Masuuli kuanzisha Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani. Madhumuni ya kitengo hiki ni kutoa ushauri kwa Afisa Masuuli juu ya utumiaji mzuri wa rasilimali. Majukumu hayo ni kama ifuatavyo:-

    1. Kukagua na kutoa taarifa kama kuna udhibiti wa kutosha kwenye makusanyo, utunzaji na matumizi ya rasilimali fedha za ofisi.
    2. Kukagua na kutoa taarifa kama mifumo ya utendaji iliyoainishwa kwenye sheria , kanuni na maelekezo mbalimbali kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali yanafuatwa ili kuhakikisha kuwa kuna udhibiti wa kutosha kwenye matumizi fedha katika ofisi.
    3. Kukagua na kutoa taarifa kama mipangilio na mgawanyo kwenye akaunti za mapato (revenue) na matumizi ni sahihi.
    4. Kukagua na kutoa taarifa juu ya usahihi wa hesabu na taarifa mbalimbali zinazoandaliwa na ofisi.
    5. Kukagua na kutoa taarifa juu ya mifumo iliyopo na inayotumika kutunza mali za serikali, pamoja na kufanya uhakiki wa mali hizo.
    6. Kupitia na kutoa taarifa juu ya shughuli au mipango ya ofisi ili kuona kama inaendana na malengo na madhumuni ya uanzishwaji wa ofisi.
    7. Kupitia na kutoa taarifa juu ya hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Menejimenti katika kujibu hoja za Mkaguzi wa Ndani; na kusaidia Menejimenti juu ya utekelezaji wa mapendekezo ya hoja hizo; na pale inapofaa kusaidia namna ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
    8. Kukagua mifumo ya TEKNOHAMA iliyopo katika ofisi na kutoa taarifa kama kuna umadhubuti wa udhibiti uliopo.
    9. Kuandaa Mpango kazi na Mpango mkakati wa ukaguzi.
    10. Kuandaa na kusimamia mipango ya ukaguzi.
    11. Kufanya ukaguzi wa thamani kwenye miradi ya kimaendeleo na ukaguzi wa thamani mbalimbali.