• Jumatatu – Ijumaa Saa 1:30Asb – 9:30Alasiri

 • WALIOTEMBELEA

 • Mipango

  KITENGO CHA MIPANGO

  MIPANGO

  Kazi kubwa ya Kitengo cha Mipango ni kusimamia na kuratibu mipango na Bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Hazina. Aidha, kulingana na muundo wa Ofisi,  kitengo kina majukumu yafuatayo:

  1. Kuratibu matayarisho ya Bajeti, Mpango wa mwaka pamoja na kufuatilia utekelezaji;
  2. Kusimamia ufuatiliaji na tathmini wa Shughuli za Msajili wa Hazina;
  3. Kuandaa michango ya Ofisi katika Hotuba ya Bajeti pamoja na taarifa ya mwaka ya Uchumi;
  4. Kuwajengea uwezo watumishi katika maeneo ya Mpango Mkakati, bajeti na mfumo wa ufuatiliaji na tathmini;
  5. Kuratibu mapitio ya Sera za Ofisi ya Msajili wa Hazina na kuzihuisha ili ziendane na Sera za kitaifa;
  6. Kupitia na kutoa ushauri juu nyaraka mbalimbali za kisera kutoka kwenye Taasisi na Mashirika ya Umma;
  7. Kutayarisha makubaliano ya Awali (MOU) kwenye miradi/Programu ili kupata fedha za nje;
  8. Kuratibu shughuli za Bunge zinazohusu utendaji wa Mashirika na Taasisi za Umma;
  9. Kutayarisha miradi ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mpango kazi na kufuatilia utekelezaji wake;
  10. Kuibua mikakati ya kutafuta rasilimali fedha za kuendesha Ofisi;
  11. Kufanya utafiti wa awali kuhusu utoaji wa huduma ili kupata maoni ya wadau juu ya huduma zitolewazo na kuishauri menejimenti; na
  12. Kuratibu mapitio ya utendaji wa nusu mwaka na wa mwaka wa Ofisi ya Msajili wa Hazina .