• Jumatatu – Ijumaa Saa 1:30Asb – 9:30Alasiri

  • WALIOTEMBELEA

  • Habari, Mawasiliano na Uhusiano

    KITENGO CHA HABARI, MAWASILIANO NA UHUSIANO

    Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano katika Ofisi ya Msajili wa Hazina kinachoundwa na wataalamu wa taaluma ya habari na mawasiliano kwa Umma, kinahusika moja kwa moja na mambo yafuatayo;

    MAJUKUMU

    1. Kushauri masuala yote ya kihabari, mawasiliano na Uhusiano wa Umma katika ofisi.
    2. Kuzalisha na kusambaza hati kama vipeperushi, makala, majarida na kadhalika kwa ajili ya kuuarifu Umma juu ya sera, utaratibu, shughuli na marekebisho yaliyofanywa na ofisi;
    3. Kuratibu mikutano mifupi ya ofisi;
    4. Kukuza shughuli na mipango/maazimio ya ofisi;
    5. Kuratibu matayarisho ya nyaraka mbalimbali kwa ajili ya semina na mikutano;
    6. Kuratibu utayarishaji na uzalishaji wa makala za ofisi na magazeti;
    7. Kuboresha na kudumisha habari katika tovuti na mitandao mingine ya kijamii iliyopo katika Ofisi ya Msajili wa Hazina;
    8. Kushauri juu ya hafla ya Gawio, Michango ya asilimia 15 na mingine kutoka katika Taasisi, Mashirika ya Umma, Wakala na Kampuni ambazo Serikali ina hisa.
    9. Kushauri Idara na Vitengo mbalimbali juu ya uzalishaji wa hati, vipeperushi na kadhalika.
    10. Kuratibu majibu ya malalamiko ya wadau kupitia vyombo mbalimbali vya habari
    11. Kuratibu ushiriki wa Ofisi ya Msajili wa Hazina katika Maonesho mbalimbali ya kitaifa, mfano Sabasaba, Nanenane, Wiki ya Utumishi wa Umma na kadhalika.