• Jumatatu – Ijumaa Saa 1:30Asb – 9:30Alasiri

  • WALIOTEMBELEA

  • TEHAMA

    KITENGO CHA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA)

    MAJUKUMU

    Katika kufanikisha majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) na kufikia malengo iliyojiwekea, Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kinawajibika kutekeleza majukumu yafuatayo ;-

    1. Kutekeleza Sera ya Teknohama ya Serikali,
    2. Kubuni na kushauri Ofisi kuhusiana na Mifumo yote ya Teknohama kwa ndani ili kuboresha utendaji;
    3. Kuendeleza na Kuratibu Mfumo Mtambuka wa Taarifa za Mashirika yaliyoratibiwa shughuli zake na Ofisi ya Msajili wa Hazina,
    4. Kuratibu na Kushauri matumizi bora ya vifaa na programu za ofisi ,
    5. Kushauri na kusaidia ununuzi wa programu na vifaa vya Tehama katika ofisi,
    6. Kuanzisha na Kuratibu matumizi sahihi ya mawasiliano kwa ndani na nje ya ofisi;
    7. Kufanya tafiti na kupendekeza maeneo ya kutumia Teknohama kama chombo cha kuboresha utoaji wa huduma kwa Taasisi na Mashirika ya Umma;
    8. Kukuza matumizi ya Teknohama katika Taasisi na Mashirika ya Umma na;
    9. Kuboresha Mawasiliano ya Ofisi kwa wadau wake kupitia wavuti yake