IDARA YA UBINAFSISHAJI NA UFUATILIAJI
MAJUKUMU
- Kufuatilia na kuhakikisha gawio kutoka Mashirika ya Umma na Taasisi ambazo Serikali ina hisa chache;
- Kusimamia na kutathmini utendaji kazi wa mashirika, taasisi za umma na Mashirika yaliyobinafsishwa;
- Kuhifadhi taarifa na kumbukumbu (database) za mashirika yaliyorekebishwa na kubinafsishwa;
- Kushughulikia madai na malalamiko ya waliokuwa wafanyakazi wa mashirika ya umma yaliyorekebishwa na kubinafsishwa;
- Kusimamia ubinafsishaji na urekebishaji wa mashirika ya umma kwa kushirikiana na Wizara mama;
- Kufuatilia na Kusimamia Mitaji (capital Grants and Capital Funds), Ruzuku, au retained earnings katika Mashirika yaliyorekebishwa na kubinafsishwa hususani pale ambapo Serikali ina Hisa.