• Jumatatu – Ijumaa Saa 1:30Asb – 9:30Alasiri

 • WALIOTEMBELEA

 • Uwekezaji wa Umma

  IDARA YA UWEKEZAJI WA UMMA

  MUUNDO NA MAJUKUMU YA IDARA:

  Idara ya Uwekezaji ina sehemu (sections) Tatu ambazo ni sehemu inayoshughulika na Mashirika ya Kibiashara (Commercial Section), sehemu ya pili inayoshughulika Mashirika yasiyo ya Kibiashara (Non Comercial Section) na Sehemu ya Tatu inayoshughulika na Mashirikia Simamizi (Regulatory Authorities)

  MAJUKUMU

  1. Kusimamia hisa za Serikali katika Taasisi na Mashirika ya Umma;
  2. Kuongeza mitaji katika Mashirika ya Umma kwa niaba ya Serikali;
  3. Kuhakikisha upatikanaji wa gawio na mapato mengine kwa Serikali kutoka Kampuni ambazo Serikali imewekeza kwa namna moja au nyingine;
  4. Kuishauri Serikali kuhusu uanzishaji wa Mashirika na Taasisi za Umma na kuyapatia mitaji au mali;
  5. Kupitia ufanisi wa fedha wa mashirika na taasisi za Umma ili kuweza kupendekeza hatua za kuchukua zenye lengo la kuyaunganisha, kuyauza au kuyavunja kwa madhumuni ya kuleta ufanisi;
  6. Kuidhinisha endapo shirika moja linataka kununua hisa katika taasisi au shirika lingine;
  7. Kuwekeza au kuuza mali za Mashirika au Taasisi za Umma;
  8. Kusimamia mfuko wa uwekezaji katika Mashirika ya Umma;
  9. Kuishauri Serikali kuhusu uanzishaji, uunganishaji au uvunjaji wa Mashirika ya Umma;
  10. Kuishauri Serikali kuhusu uwekezaji katika Mashirika ya Umma;
  11. Kuishauri Serikali kuhusu uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji wakuu wa Mashirika ya Umma;
  12. Kuishauri Serikali kuhusu njia ya kuyasaidia mashirika yenye matatizo ya kipekee;
  13. Kutathmini utendaji kazi wa Mashirika ya Umma kwa kuzingatia vigezo vya utendaji kazi vilivyowekwa;
  14. Kuidhinisha viwango vya ada na posho za Bodi za Wakurugenzi;
  15. Kuidhinisha kanuni za fedha katika Mashirika na taasisi za Umma;
  16. Kukagua utendaji wa Mashirika.

  [vc_custom_heading text=”Matukio Mbalimbali” font_container=”tag:h2|font_size:18|text_align:left|color:%23ffffff” google_fonts=”font_family:Acme%3Aregular|font_style:400%20regular%3A400%3Anormal” css=”.vc_custom_1588321000280{margin-top: 0px !important;border-bottom-width: 6px !important;padding-top: 5px !important;padding-bottom: 5px !important;padding-left: 22px !important;background-color: #1e73be !important;}”]

  [vc_empty_space height=”31px”][vc_custom_heading text=”Pata Matukio Zaidi” font_container=”tag:h2|font_size:18|text_align:center|color:%231e73be” google_fonts=”font_family:Acme%3Aregular|font_style:400%20regular%3A400%3Anormal” link=”url:https%3A%2F%2Fwww.tro.go.tz%2Fsw%2Fcategory%2Fmatukio%2F%20|||” css=”.vc_custom_1588321368722{margin-top: -10px !important;}”]