Agosti 20, 2023 kupitia wasilisho lake katika kikao kazi hicho, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu alisema, ofisi hiyo inafanya mageuzi katika muundo na utaratibu wa kusimamia mashirika na taasisi za umma.

Mchechu alisema, pamoja na mambo mengine imependekeza kuanza utaratibu wa kuajiri na kufukuza watendaji wakuu wa mashirika hayo.

“Sasa haya tunayotaka kuyafanya tumeyakopa kutoka baadhi ya nchi,China tulikuwa tunaangalia wanafanyaje,TR (Ofisi ya Msajili wa Hazina) wanafanyaje, wao wanaita SASAC (State-owned Assets Supervision and Administration Commission of the State Council (SASAC).”

Mchechu ameyabainisha hayo Agosti 20,2023 mbele ya Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma katika siku ya pili ya kikao kazi kinachoendelea jijini Arusha.

SASAC ambayo ilianzishwa mwaka 2003 na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ina jukumu la kusimamia biashara zinazomilikiwa na Serikali (SOEs), ikijumuisha kuteua watendaji wakuu na kuidhinisha muunganisho wowote au mauzo ya hisa au mali, pamoja na kuandaa sheria zinazohusiana na SOEs.

“Ni bodi imara, inasimamia makampuni yao makubwa, lakini nimeangalia sheria yao, wajibu wao hautofautiani kabisa na wajibu wetu sisi tulionao.

“Wanatakiwa wasimamie mali zinazomilikiwa na Serikali, hicho ndicho tunachotakiwa kukifanya Tanzania, wanasimamia uwekezaji unaofanywa na mashirika na kudhibiti utendaji wake, ndivyo Sheria ya TR inavyotuambia tufanye, kuandaa sera zinazodhibiti mapato na matumizi ya mashirika, ndiyo TR tunvyofanya Tanzania.

“Kusimamia mageuzi na mifumo ya utendaji katika mashirika ikiwa ni pamoja na kukuza mfumo wa kisasa wa uanzishwaji wa biasha, ndiyo TR tunavyofanya Tanzania, kuendesha marekebisho ya kimkakati ya kimpangilio na muundo wa uchumi, ndiyo TR tunatakiwa tufanye Tanzania.

“Kuteua na kuwaondoa watendaji wakuu wa mashirika,labda hili sisi ndiyo hatulifanyi.Tunapendekeza sasa ili tuweze kufanya vizuri.

“Kwa hiyo ukiangalia yote haya SASAC wanayafanya, tunayo sisi TR, lakini ni kwamba hatujacheza mpira kwa viwango.

“Ni kama ambavyo timu zetu za Simba na Yanga wana sheria zile zile 17 za FIFA na zile timu zetu za daraja la kwanza sijui premium league, lakini mpira wetu ndiyo huo huo.

“Tumeenda kuangalia Kuwait nayo ukiangalia, Singapore ni kitu hicho hico, kwa hiyo tunajaribu kubuni mifumo ambayo itaenda na itasomana pia na wenzetu, ndiyo maana tunaangalia wenzetu wamefanya nini na mafanikio yao yamekuwaje, lakini kuna mafanikio makubwa.

“Kuna mafanikio ya kuwezesha kukuwa kwa kasi kwa sekta zao, kukuza miradi mikubwa, kuvutia wawekezaji na mengine mengi.”

Amesema kuwa, azimio hilo ni moja ya mapendekezo ya kuboresha ofisi hiyo ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema ameyapitisha