• Jumatatu – Ijumaa Saa 1:30Asb – 9:30Alasiri

  • WALIOTEMBELEA

  • Kuhusu Idara

    IDARA YA HUDUMA NA USHAURI WA KIMENEJIMENTI

    MAJUKUMU

    1. Kuwezesha maandalizi na mapitio ya Miundo ya Taasisi na masuala ya Rasilimali Watu katika Taasisi na Mashirika ya Umma na kushauri ipasavyo;
    2. Kushauri kuhusu Maendeleo ya Rasilimali Watu katika Taasisi na Mashirika ya Umma;
    3. Kufanya ukaguzi wa Kimenejimenti katika Taasisi na Mashirika ya Umma na kuandaa ripoti,
    4. Kushauri na kupitia nyenzo za Utendaji za Taasisi na Mashirika ya Umma na kuhakikisha zinatekeleza maelekezo ya Msajili wa Hazina pamoja na miongozo mingine kutoka Serikali Kuu.
    5. Kushauri juu ya mifumo ya usimamizi ya kiutendaji inayotumika katika Taasisi na Mashirika ya Umma.
    6. Kuandaa na kutoa Nyaraka, Miongozo na Maelekezo mbalimbali kuhusu utendaji na masuala yanayohusu kuboresha tija katika Taasisi na Mashirika ya Umma.
    7. Kuchambua na Kuidhinisha Muundo wa Taasisi, Miundo ya Utumishi, Kanuni za Utumishi, Mikataba ya hiari, Ikama na Bajeti za Taasisi za Serikali, Mishahara na marupurupu ya wafanyakazi wa Mashirika na Taasisi za Umma yanayozingatia tija, ufanisi, kukua kwa mtaji (wekezo) na kulipwa gawio na ziada Serikalini.