• Jumatatu – Ijumaa Saa 1:30Asb – 9:30Alasiri

 • WALIOTEMBELEA

 • Ununuzi na Ugavi

  KITENGO CHA MENEJIMENTI YA USIMAMIZI WA UNUNUZI

  MAJUKUMU

  Kitengo cha Menejimenti ya Usimamizi wa Ununuzi (PMU) ni moja ya vitengo vilivyopo katika Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) kikiwa na wajibu wa kusimamia unununi kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi ya Umma Na. 7 ya Mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013.

  Kwa mujibu wa Muundo wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (Organisation Structure) na Sheria ya Ununuzi ya Umma Na.7 ya Mwaka 2011 na Kanuni zake za mwaka 2013, Kitengo cha Menejimenti ya Usimamizi wa Ununuzi kina majukumu yafuatayo;

  1. Kusimamia majukumu yote ya ununuzi na Uuzaji kwa njia ya zabuni;
  2. Kusaidia kazi zinazofanywa na bodi ya zabuni;
  3. Kutekeleza maamuzi ya bodi ya zabuni;
  4. Kuandaa mpango wa ununuzi na kusimamia utekelezaji wake;
  5. Kuangalia na kuandaa taarifa ya mahitaji;
  6. Kuandaa matangazo ya zabuni;
  7. Kuandaa hati ya zabuni na taarifa yake;
  8. Kutoa mikataba iliyoidhinishwa kwa wazabuni;
  9. Kutunza na kuhifadhi kumbukumbu ya ununuzi na uuzaji;
  10. Kuandaa na kuhifadhi rejista ya mikataba ya wazabuni wanaoshinda zabuni; na
  11. Kuandaa taarifa za kila wakati zinazofanyika katika stoo kuwezesha uhakiki wa mali na utunzaji katika stoo.