MAJUKUMU YA UTAWALA NA RASILIMALI WATU
- Kusimamia Rasilimali Watu na majukumu ya kiutawala katika Ofisi ya Msajili wa Hazina,
- Kuratibu taratibu za ajira, malipo, tathmini ya utendaji, promotions, ustawi wa wafanyakazi, motisha, mahitaji ya mafunzo, terminations, stahiki na kuhakikisha kwamba Kanuni za Utumishi zinafahamika na kufuatwa,
- Kutafsiri Kanuni za Utumishi wa Umma, Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma, Sheria za Kazi na kanuni zake, na kuhakikisha kwamba zinazingatiwa na kutekelezwa,
- Kuhakikisha kwamba kuna mahusiano mazuri katika eneo la kazi na kwamba migogoro yote inatatuliwa mara moja na ipasavyo,
- Kuhakikisha kwamba Msajili wa Hazina ana mfumo bora wa utoaji tuzo kwa watumishi, sera za malipo na kuhakikisha kwamba kuna taratibu bora za kuwahamasisha watumishi,
- Kutoa ushauri juu ya maendeleo ya watumishi, usimamizi wa utendaji na usimamizi wa kazi kwa watumishi wa Msajili wa Hazina;