JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA

 

TANGAZO LA MNADA

 

 

 

03/01/2023

Wananchi wote mnatangaziwa kwamba, Ofisi ya Msajili wa Hazina itauza kwa njia ya Mnada wa Hadhara vifaa mbalimbali chakavu katika ofisi za Msajili wa Hazina zilizoko kwenye jengo la CHC Samora Mkoa wa Dar es Salaam kama inavyooneshwa hapa chini;

  1. MKOA WA DAR ES SALAAM
TAREHE KITUO AINA YA MALI
28/01/2023 Ofisi ya Msajili wa Hazina

Jengo la CHC

Samora Avenue

Vifaa mbalimbali chakavu

 

MASHARTI YA MNADA

  1. Kifaa kitauzwa kama kilivyo mahali kilipo;
  2. Mnunuzi atalazimika kulipa papo hapo gharama isiyopungua asilimia mia (100%) ya thamani ya chombo / kifaa alichonunua siku ya mnada. Mnunuzi akishindwa kutimiza sharti hili atakosa haki zote za ununuzi wa chombo/kifaa husika na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani ataonekana kama mwenye kutaka kuharibu mnada
  3. Mnunuzi atatakiwa kuondoa/kuchukua kifaa alichonunua katika muda wa siku saba (7) kuanzia siku ya kukamilisha malipo;
  4. Ruhusa ya kuangalia vyombo itatolewa kwa siku mbili (2) tarehe 25-26 Januari, 2023 kabla ya tarehe ya mnada utakaofanyika tarehe 28 Januari, 2023 kuanzia saa 3 mpaka saa 7 Mchana; na
  5. Mnada utaanza saa Nne (04:00) asubuhi katika Ofisi ya Msajili wa Hazina iliyopo Mtaa wa Samora.

 

Msajili wa Hazina

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA