• Jumatatu – Ijumaa Saa 1:30Asb – 9:30Alasiri

  • WALIOTEMBELEA

  • WAKULIMA WA MIWA WA KILOMBERO KUNUFAIKA NA UPANUZI WA KIWANDA CHA SUKARI CHA KILOMBERO

    Serikali kwa kushirikiana Kampuni ya Kiwanda cha Sukari cha Kilombero imeanza utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa upanuzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha sukari kwa tani 139,000 kutoka viwango vya sasa vya tani 127,000 kwa mwaka, hadi kufikia tani 271,000 ifikapo mwaka 2023.

     

    Kampuni ya Kiwanda cha Sukari cha Kilombero inayomilikiwa na Kampuni ya Illovo Sugar Africa  kwa Asilimia 75 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Msajili wa Hazina kwa asilimia 25 imeanza maandalizi ya Mradi huo wa upanuzi wa kiwanda hicho utakaogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 584.

     

    Akizungumza wakati wa ziara ya Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto kiwandani hapo, Meneja Mkuu – Fedha, Fakihi Fadhili alisema mradi wa upanuzi wa kiwanda hicho utaongeza usambazaji wa miwa kutoka kwa wakulima wadogo wa Bonde la Mto Kilombero kutoka tani 600,000 cha hivi sasa mpaka kufikia tani 1,700,000 kwa kuwa Mradi wa upanuzi wa kiwanda umezingatia hali ya ongezeko la miwa kwa sasa na nautawezesha miwa yote iliyopo kuchakatwa kila mwaka, lengo likiwa ni kupunguza usumbufu na upotevu unaosababishwa mara kwa mara hasa kipindi cha mvua.

     

    Mradi wa upanuzi wa kiwanda hicho utaongeza maradufu la kiwango cha miwa kutoka kwa wakulima wa nje na hivyo kuongeza mara tatu ya kipato cha wakulima hao kufikia Shilingi bilioni 300 ifikapo mwaka 2028, aidha idadi ya wakulima wadogo wadogo watakaosambaza miwa kwa kiwanda kipya itaongezeka kutoka 8,000 hadi 14,000 – 16,000, na hivyo kugusa moja kwa moja zaidi ya wananchi 100,000 wa maeneo yanaozunguka bonde la Kilombero na kujishughulisha na uzalishaji wa sukari alisisitiza Fakihi.

     

    Kwa upande wa ajira, Fakihi alisema kuwa kutakuwa na ongezeko la ajira ya moja kwa moja ya zaidi ya  watu 2,000 kutokana na upanuzi wa kiwanda na uzalishaji wa miwa vilevile jumla ya kodi ya shilingi bilioni 50 zinazolipwa sasa na Kampuni ya Sukari ya Kilombero inakadiriwa kuongezeka mara tatu kutokana na upanuzi na ufanisi wa biashara mpaka kufikia mwaka 2028

     

    Mradi huo unatarajiwa kutazalisha umeme kwa ajili ya matumizi ya kiwanda na hata kuelekeza umeme mwingine kwenye gridi ya taifa kuiuzia TANESCO. Vilevile, mradi utaboresha ufanisi katika uzalishaji kwa kupunguza gharama za uendeshaji, kwani vifaa na vipuri chakavu vitabadilishwa na hivyo kuimarisha uwezo wa usindikaji.

     

    Aidha, inatazamiwa kuwa mchango wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero kwa uchumi wa nchi utaongezeka maradufu kutoka kiasi cha sasa cha shilingi bilioni 340 kwa mwaka hadi kufikia wastani wa shilingi bilioni 750 kiwanda kipya kitakavyoanza uzalishaji.

     

    Akizungumza wakati wa ziara hiyo Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto aliishukuru Kampuni ya Sukari ya Kilombero na Menejimenti yake kwa kuunga mkono juhudi za Serikali (mwekezaji mwenza katika mradi huo kupitia hisa zake asilimia 25) katika uwekezaji huu wa kihistoria unaolenga kuongeza uzalishaji wa Sukari Nchini na kupunguza kiwango cha pengo la sukari ambayo inapaswa kuingizwa nchini kila mwaka. Aidha Mgonya  alitoa wito wa kuongeza juhudi katika utendaji kazi, kuimarisha usimamizi wa mradi na kuahidi kutoa ushirikiano utakaohitaji katika kufanikisha mradi huu muhimu kwa uchumi wa Taifa.

    Matukio Mbalimbali

    Pata Matukio Zaidi