Serikali, kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, inasimamia jumla ya Mashirika ya Umma na ya Kisheria 253 (PSCs). Kati ya haya, 218 ni watoa huduma, huku 35 yakifanya shughuli za kibiashara.
Uangalizi wa PSCs 253, ambapo idadi kubwa ziko kwaajili ya utoaji wa huduma, unaakisi umuhimu wa sekta ya umma katika uchumi wa nchi.
Wakati mashirika haya yana jukumu muhimu katika utoaji wa huduma, taasisi za kibiashara zinatoa fursa ya kimkakati kwa ajili ya ukuaji wa uchumi na uzalishaji wa mapato.