Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA

Majukumu

Sheria ya Msajili wa Hazina Na. 370 na marekebisho yake na sheria zingine zinazoongoza Ofisi ya Msajili wa Hazina, kazi na wajibu wa Ofisi hii zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni:

  1. Kutunza  hazina na rasilimali za Taasisi za Umma  kwa niaba ya Serikali (Jukumu la Usimamizi);
  2. Kuishauri Serikali kuhusu masuala ya uwekezaji na usimamizi wa Taasisi za Umma na Mashirika yaliyoundwa Kisheria (Jukumu la Kutoa Ushauri); na
  3. Udhibiti na ufuatiliaji wa utendaji wa Taasisi za Umma na Mashirika yaliyoundwa Kisheria  (Jukumu la Ufuatiliaji na Usimamizi wa Sheria).

Hivyo, kwa ujumla wajibu wa ofisi hii ni kama ifuatavyo:

  • Msajili wa Hazina ana mamlaka ya kusimamia shughuli zote, rasilimali zote za mashirika ya umma,  taasisi na wakala wa serikali, kupitia matumizi ya pesa katika mashirika ya umma na yaliyoundwa kisheria  kwa lengo la kupendekeza hatua zinazolenga kuunganisha, kuvunja au kuboresha utendaji wake
  • Kuweka mifumo, sheria na mikakati ya kuboresha utendaji wa menejimenti;
  • Kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu uanzishwaji wa mashirika mapya ya umma au ya kisheria, kuimarisha, kuvunja na kuwekeza katika shirika (business) au eneo (property) katika Taasisi hizo kwa lengo la kuleta ufanisi na kushauri namna ya kuyasaidia mashirika matatizo mahususi;
  • Kuweka malengo ya kifedha na vigezo vingine vya kiutendaji (Viashiria vya Kiutendaji)  vya kuzingatiwa na mashirika ya umma na yaliyoanzishwa kisheria;
  • Uteuzi wa Bodi ya Wakurugenzi, kutathmini ufanisi wake na kupendekeza kwa Serikali namna ya kuboresha utendaji wake;
  • Kuwekeza au kuvunja miradi katika mashirika ya umma au yaliyoundwa kisheria baada ya kushauriana na Serikali;
  • Kufuatilia na kuhakikisha magawio kutoka katika mashirika ya umma na mashirika yaliyoundwa kisheria  ambako Serikali ina hisa yanalipwa kwa wakati;
  • Kuidhinisha uanzishwaji, utumiaji na uboreshaji wa sheria za fedha  ili kuhakikisha kuwa kuna usahihi katika mapato na matumizi katika taasisi za umma na mashirika yaliyoanzishwa kisheria ;
  • Kutathmini na kupitisha miundo ya pahala pa kazi na mishahara, aina za huduma na upandaji vyeo (scheme of service), motisha, mikataba ya hiari, magawio kwa serikali, tataribu na sheria kwa wafanyakazi wa taasisi na mashirika yaliyoanzishwa kisheria;
  • Kujadili, kutoa mapendekezo na kupitisha  mipango ya mwaka ya taasisi za umma na mashirika  yaliyoanzishwa kisheria au vyombo vingine vya serikali ambavyo kwavyo Msajili wa Hazina  anahusika  kabla ya kuwasilishwa Serikalini  kwa ajili ya kuunganishwa katika  mipango ya jumla ya kiuchumi ya Serikali  kwa ajili ya kupanga bajeti na malengo ya mwaka mzima;
  • Kuzisimamia taasisi za umma na mifuko ya uwekezaji ya mashirika yaliyoanzishwa kisheria;
  • Kutathmini  kila mara utendaji na ufanisi wa bodi  na kamati za  menejimenti za Mashirika ya Umma na mashirika yaliyoanzishwa kisheria  na kupendekeza hatua za kuchukuliwa na Serikali ili kusahihisha au kuboresha ili kuhakikisha kunakuwa na matumizi sahihi na bora zaidi ya fedha na rasilimali  za mashirika hayo;
  • Kufuatilia na kutathmini programu za mafunzo  katika taasisi za umma na mashirika yaliyoanzishwa kisheria;
  • Kufuatilia mikopo ya kuzalishia mali, ruzuku, mifuko ya kuzalisha mali, hazina, mapato yaliyotokana na mashirika na uwekezaji mwingine wowote wa umma;
  • Kuandaa na kutoa ilani  na miongozo ili kuongeza ufaafu na ufanisi katika taasisi za umma na mashirika yaliyoanzishwa kisheria;
  • Kupitisha iwapo shirika la umma lenye kusudio la kununua hisa  au linakusudia kuwekeza katika shirika jingine lolote  au kampuni  ya umma  linaweza kufanya hivyo;
  • Kuukilia  namna shirika mahususi lililorekebishwa  au kuanzishwa kisheria linavyoweza kupanuliwa kwa kushirikiana na Wizara husika/ mama ;
  • Kuandaa na kusaini mikataba na mashirika ya umma au yaliyoanzishwa kisheria  ambayo kwayo utoaji wa gawio  na michango kwenye kapu la  Serikali  ni kiashiria kikuu cha utendaji  bora wa shirika hilo;
  • Kuimarisha  uwajibikaji  na utendaji wa mashirika ya umma  na yaliyoanzishwa kisheria  ili kuongeza uwezo wake  wa kuongeza mapato, kupunguza matumizi  yasiyokuwa na faida na kuongeza faida;
  • Kuendesha ukaguzi wa mara kwa mara wa menejimenti ya taasisi za umma  na mashirika yaliyoanzishwa kisheria  ili kubainisha mapungufu na kuishauri Serikali   iapasavyo;
  • Kufanya tathmini  na kufuatilia mashirika yaliyobinafsishwa;
  • Kusimamia urekebishaji wa mashirika ya umma na mashirika yaliyoanzishwa kisheria;
  • Kusimamia hatua  za awali za utoaji wa hisa za serikali kwa wananchi katika masoko ya hisa;
  • Kukusanya madeni kutoka katika mashirika ya umma yatokanayo makubaliano ya kuuziana;
  • Kufuatilia hati miliki za mashirika mbalimbali ya umma, mashirika yaliyoanzishwa kisheria ; na
  • Kufanyia kazi majukumu mengine ya mashirika mfu ambayo ni Loans and Advances Realization Trust (LART), Air Tanzania Holding Corporation (ATHCO), Simu 2000 Ltd, National Bank of Commerce (X-NBC), Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma,  na Consolidated Holding Corporation.