Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA

Ofisi ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ‘Sabasaba’ kutangaza huduma
01 Jul, 2025
Ofisi ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho  ‘Sabasaba’ kutangaza huduma

Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina imetoa rai kwa taasisi za umma kutumia maonesho ya 49 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam  maarufu kama Sabasaba kama jukwaa la kutangaza huduma zinazotolewa na serikali.

 

Akizungumza Jumatatu, Julai 1, 2025, katika viwanja vya Sabasaba, Bw. Sabato Kosuri, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina, alisema wananchi ndio wamiliki wa taasisi za umma na hivyo wanahaki ya kujua uwekezaji uliofanyika.

 

Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imewekeza kiasi cha Sh86.25 trilioni katika taasisi za umma na kampuni ambazo Serikali ina umiliki wa hisa chache.

 

Kati ya kiasi hicho Sh83.33 trilioni zimewekezwa kwenye taasisi 152 ambazo serikali ina hisa nyingi, huku Sh2.82 trilioni zikiwekezwa kwenye kampuni 56 ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache.

 

 

Bw. Kosuri alisema Maonesho ya biashara ya Sabasaba ni mwendelezo wa tafsiri ya ndoto ya Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuongeza ufanisi wa taasisi za umma lengo likiwa ni kuleta tija na rejesho halisi la uwekezaji uliofanywa katika taasisi za umma.  

 

“Sisi kama wasaidizi wa Mhe. Rais tumedhamiria kutengeneza mazingira ya uwajibikaji kwani taasisi za umma ni mali za umma  na hivyo zinawajibika moja kwa moja kwa umma,” alisema.

Bw. Kosuri alisema ushiriki wa Ofisi ya Msajili wa Hazina na taasisi inazozisimamia katika maonesho ya Sabasaba utawapa fursa kwa wadau na wananchi kwa ujumla kuuliza maswali na kutoa maoni.

 

“Tutumie maonesho ya Sabasaba kama jukwaa la kupokea maoni na kuwaambia wadau na wananchi kwa ujumla mambo ambayo serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais. Dk. Samia Suluhu Hassan inayafanya,” alisema Bw. Kosuri.

 

 ili kuzungumza na wadau na wananchi pamoja na kupokea maoni pamoja na kuwaelezea mambo yaliyo na yanayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita.

 

Alihitimisha kwa kuwakaribisha wadau mbalimbali na wananchi wote katika banda namba 39 la Ofisi ya Msajili wa Hazina lililopo katika  ukumbi wa Kilimanjaro.