Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA

Ofisi ya Msajili wa Hazina yaimwagia sifa STAMICO
24 Jun, 2025
Ofisi ya Msajili wa Hazina yaimwagia sifa STAMICO

 

Na Mwandishi wa OMH

Dodoma. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) imelimwagia sifa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kujitegemea kwa asilimia 100 huku likiendelea kutoa gawio kwa Serikali.

 

Sifa hizo zilitolewa jijini Dodoma, Jumanne, Juni 24, 2025, na Bw. Richard Mayongela, Mkurugenzi Msaidizi wa mashirika yanayofanya biashara kutoka OMH.

 

 Bw. Mayongela alikuwa anazungumza wakati wa uzinduzi wa mitambo ya wachimbaji wadogo na vitendea kazi vya STAMICO.

 

 “Kwa hatua iliyofikia hivi sasa, STAMICO linaweza kujitegemea kwa asilimia mia moja na bado likawasilisha gawio serikalini,” alisema huku akisema mafanikio hayo yanatokana na maboresho yaliyofanywa ndani ya shirika hilo.
 

Hili sio jambo rahisi kwa mashirika kuwasilisha asilimia 80 ya mapato yake kwenye miradi ya maendeleo na kisha kutumia asilimia 20 pekee kujiendesha.”

 

Tafsiri yake ni, pamoja na mambo mengine, shirika hilo (STAMICO) inaweza ikasimamia shughuli zake za ulipaji wa mishahara kwa asilimia 100 na hivyo kuipunguzia serikali mzigo.

 

 “Zamani  Serikali ilikuwa inabeba mzigo wa mishahara na fedha za miradi ya maendeleo. Kwasasa hadithi imebadilika kwa baadhi ya taasisi ikiwemo STAMICO inayotenga kati ya asilimia 80-82 ya mapato yake ya ndani na kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.” Alisema Bw. Mayongela.

 

Kutokana na mageuzi hayo, serikali inaelekeza rasilimali fedha zilizopo kwenye miradi mingine ya maendeleo.