Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA

Msajili wa Hazina afanya mazungumzo na TRC, LATRA
04 Sep, 2025
Msajili wa Hazina afanya mazungumzo na TRC, LATRA

Na Mwandishi wa OMH

 

Dodoma. Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Shiwa, pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Bw. Abdallah Mhagama.

 

 

Mazungumzo hayo, ambayo pia yalihusisha wataalamu kutoka taasisi hizo tatu, yalifanyika katika ofisi za LATRA jijini Dodoma, Jumatano, Septemba 3, 2025, na yalilenga kuboresha utendaji kazi wa TRC.

 

Ofisi ya Msajili wa Hazina inasimamia jumla ya taasisi na kampuni 308 ambazo Serikali ina hisa.

 

Kati ya hizo, taasisi 252 – zikiwemo TRC na LATRA – ni zile ambazo Serikali inamiliki hisa nyingi, huku 56 zikiwa ni kampuni ambazo Serikali inamiliki hisa chache.