SERIKALI kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, imetangaza kuuza kwa njia ya zabuni mali za viwanda sita vinavyomilikiwa na Serikali. Hii ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika uendelezaji wa viwanda nchini.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, viwanda ambavyo mali zake zimewekwa sokoni ni pamoja na Kiwanda cha kukoboa Mpunga cha Kilimanjaro Paddy Hulling Company Ltd kilichopo mkoani Kilimanjaro na Polysacks Company Limited cha Dar es Salaam.
Vingine ni NMC Mzizima cha jijini Dar es Salaam ambacho ni mahsusi kwa usagaji wa nafaka hasa mahindi. Pia vimo NMC Isaka cha Shinyanga na NMC Tabora cha mkoani Tabora vinavyojihusisha na ukoboaji wa mpunga.
Kiwanda kingine ni cha kutengeneza dawa za kuua wadudu cha Pesticides Manufacturers Limited kilichopo mkoani Kilimanjaro.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali ingia katika kiunganishi hapo chini:

PURCHASE OF ASSETS FOR SIX (6) GOVERNMENT OWNED FACTORIES