Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto akabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Dar es Salaam.  Benedicto ameteuliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Msajili wa Hazina kuchukua nafasi ya Mbuttuka ambaye ameteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali.