“Wakulima wa Miwa wa Kilombero watakuwa wanufaika wakuu kwani ongezeko kubwa la usambazaji wa miwa utahitajika kuendesha kiwanda baada ya upanuzi”

Kampuni ya Kiwanda cha Sukari cha Kilombero ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Illovo Sugar Africa  kwa Asilimia 75 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Msajili wa Hazina kwa asilimia 25, imetangaza kuidhinishwa kwa Mradi wa Upanuzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero.

Mradi wa upanuzi wa kiwanda hicho utagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 571.6. Ili kuendana na Sera na Mipango ya Nchi Mradi huu utaongeza uzalishaji wa sukari kwa tani 144,000 kutoka viwango vya sasa vya tani 127,000 kwa mwaka, hadi kufikia tani 271,000 ifikapo mwaka 2023.

Sababu za kuidhinishwa kwa mradi wa upanuzi wa kiwanda hicho ni pamoja na matarajio ya ongezeko la usambazaji wa miwa kutoka kwa wakulima wadogo wa Bonde la Mto Kilombero kutoka tani 600,000 cha hivi sasa mpaka kufikia tani 1,700,000. Hivyo, Mradi wa upanuzi wa kiwanda umezingatia ongezeko la miwa kwa sasa nautawezesha miwa yote iliyopo kuchakatwa kila mwaka ifikapo mwishoni mwa Desemba, lengo likiwa ni kupunguza usumbufu na upotevu unaosababishwa mara kwa mara hasa kipindi cha mvua.

Mradi wa Upanuzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero umekuwa kwenye mipango ya muda mrefu, pamoja na malengo ya kuongeza uzalishaji wa sukari na kukidhi mahitaji ya watumiaji,. Mradi pia utahusisha ujenzi wa vifaa vya ziada vya kuhifadhia wa sukari na vifungashio ili kupunguza gharama na kuongeza uwezo wa kampuni kuchapa vifungashio vyake.

Aidha, mradi utazalisha umeme kwa ajili ya matumizi ya kiwanda na hata kuelekeza umeme mwingine kwenye gridi ya taifa kuiuzia TANESCO. Vilevile, mradi utaboresha ufanisi katika uzalishaji kwa kupunguza gharama kubwa kwa kiasi kikubwa, kwani vifaa na vipuri chakavu vitabadilishwa na hivyo kuimarisha uwezo wa usindikaji.

Ongezeko la kilolita 4,000 katika uzalishaji wa ethanoli kwenye kiwanda cha ethanoli, italeta kiwango cha uzalishaji wa kilolita 16,000 kwa mwaka ili kukidhi mahitaji ya ndani na yale ya Afrika Mashariki.

Mradi huo umeidhinishwa na wanahisa wote wakati wa Mkutano Maalumu wa Wanahisa uliofanyika Mei 14, jijini Dar es Salaam, Tanzania. Katika mkutano huo, Illovo Sugar Africa iliwakilishwa na Bwana Gavin Dalgleish na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliwakilishwa na Msajili wa Hazina, Bwana Athumani S. Mbuttuka.

Kuidhinishwa kwa Mradi huo inaonesha kuunga mkono kwa Kampuni ya British Foods, inayomiliki Kampuni ya Illovo Sugar Africa, na imani kubwa iliyonayo kwa Kampuni ya Illovo Sugar Africa inayokuwa hasa kwenye soko la Sukari barani africa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Sukari ya Kilombero, Balozi Ami Mpungwe anasema: “Dhamira kubwa ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji kwa sekta binafsi hususan sera na hatua za makusudi za Serikali katika kulinda viwanda vya ndani vya sukari, kimekuwa kichocheo kikubwa kwa  wanahisa kuunga mkono na kuidhinisha mradi huu hapa nchini.”

Faida za kiuchumi katika kipindi baada ya utekelezaji wa mradi huo zinatarajiwa kuwa:

  • Ongezeko maradufu la kiwango cha miwa kutoka kwa wakulima wa nje na kuongeza mara tatu ya kipato cha wakulima hao kufikia Shilingi bilioni 270 ifikapo mwaka 2028;
  • Idadi ya wakulima wadogo wadogo wanaosambaza miwa kwa kiwanda kipya itaongezeka kutoka 7,500 hadi 14,000 – 16,000, na hivyo kugusa moja kwa moja zaidi ya wananchi 50,000 wa maeneo yanaozunguka bonde la Kilombero na kujishughulisha na uzalishaji wa sukari;
  • Kutakuwa na ongezeko la ajira ya moja kwa moja ya zaidi ya watu 2,000 Kutokana na upanuzi wa kiwanda na uzalishaji wa miwa;
  • Jumla ya kodi ya shilingi bilioni 66.8 zinazolipwa sasa na Kampuni ya Sukari ya Kilombero inakadiriwa kuongezeka mara tatu kutokana na upanuzi na ufanisi wa biashara mpaka kufikia mwaka 2028; na
  • Aidha, inakatazamiwa kuwa mchango wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero kwa uchumi wa nchi utaongezeka maradufu kutoka kiasi cha sasa cha shilingi bilioni 340 kwa mwaka hadi kufikia wastani wa shilingi bilioni 750 kiwanda kipya kitakavyoanza uzalishaji.

Akizungumza kwa niaba ya mbia wa Kilombero, Illovo Sugar Africa, Gavin Dalgleish alisema uwekezaji wa Illovo katika mradi huo wa upanuzi wa kiwanda ndio uwekezaji mkubwa zaidi uliowahi kufanywa nao katika bara zima la Afrika.

“Tunajivunia sana kushirikiana na watu wa Tanzania katika uwekezaji huu wa kihistoria unaolenga kupunguza kiwango cha pengo la sukari ambayo inapaswa kuingizwa nchini kila mwaka na kukidhi mahitaji ya matumizi. Kwa kupunguza uagizaji wa sukari kwa tani 144,000, makadirio yetu ni kwamba Tanzania itaokoa dola milioni 71 kila mwaka, ”alisema Dalgleish.

Ujenzi wa mradi inatarajiwa kuchukua miezi 25 na unatarajiwa kukamilika Julai 2023.

Bodi ya Kampuni ya Sukari ya Kilombero na Menejimenti inapenda kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (mwekezaji mwenza katika mradi huo kupitia hisa zake asilimia 25), Illovo Sugar Africa na wakulima wa Kilombero kwa ushirikiano na kuunga mkono mradi huu tangu kuanzishwa kwake. Aidha, Kampuni inawashuru wafanyakazi wake na wadau wengine wengi, washirika, wateja na watoa huduma ambao wamekuwa wakihimiza na kusaidia kufanikisha mipango ya upanuzi wa kiwanda.

Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kinamilikiwa na Kampuni ya Illovo Sugar kwa asilimia 75 huku Serikali ya Tanzania ikimiliki asilimia 25.

———————Mwisho————————–

 

Dokezo kwa Wahariri:

Upembuzi yakinifu uliofanywa mara mbili kuhusu upanuzi wa uzalishaji wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero ulianza mwishoni mwa mwaka 2017, na kuainishwa katika Ajenda ya Serikali ya Maendeleo ya Nchi ambayo inataka utoshelevu wa sukari nchini ifikapo 2025.

Kampuni ya Sukari ya Kilombero imefanya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya Dola za Marekani milioni 166 katika biashara katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. Uwekezaji huo umehusisha upanuzi wa uzalishaji wa miwa na sukari pamoja na uwekezaji katika kiwanda cha kisasa chenye uwezo wa kusambaza lita milioni 12 za pombe yenye ubora wa juu.

Illovo Sugar Africa, ambayo inamilikiwa na Kampuni ya British Foods ya Nchini Uingereza kwa asilimia 75 ya mtaji wa hisa uliotolewa kwa Kampuni ya Sukari ya Kilombero, na kiasi cha asilimia 25 cha hisa zinamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Kilombero ipo katika Mkoa wa Morogoro katikati/kusini mwa nchi ya Tanzania. Inajumuisha maeneo mawili ya kilimo na viwanda vya sukari ambayo ni Msolwa na Ruembe. Inazalisha sukari ya kahawia maarufu kwa chapa ya ‘B