Ofisi ya Msajili wa Hazina na IFC wajadili fursa za ushirikiano
10 Nov, 2025
Na Mwandishi wa OMH
Dar es Salaam. Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ameongoza kikao kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) na IFC, taasisi ya Benki ya Dunia inayohusika na uwekezaji katika sekta binafsi.
Kikao hicho kilichofanyika Novemba 10, 2025, jijini Dar es Salaam kililenga kujadili maeneo ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika kuendeleza uwekezaji wenye tija kwa taifa.
Kikao hicho kilihusisha menejimenti ya OMH pamoja na maofisa wa IFC wakiongozwa na Bi. Martine Valcin, Meneja wa IFC nchini Tanzania, na Bi. Aida Sykes, Afisa wa taasisi hiyo.
Ushirikiano kama huu unaendelea kuimarisha nafasi ya Tanzania katika kukuza uwekezaji wa kimkakati unaochochea maendeleo ya uchumi wa taifa.